Monday 11 November 2013

Uhuru wa Kenya amjibu JK

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akimsindikiza  mgeni wake Waziri mwenza wa Kenya, Amina Mohammed baada ya waziri huyo kumaliza  kuzungumza na waandishi wa habari Dar Salaam jana. Picha na Emmanuel Herman. 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Novemba11  2013  saa 10:0 AM
Kwa ufupi
  • Kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje wa Kenya, Amina Mohamed, Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu akisema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania na kwamba  walijiingiza katika mazungumzo yake na Uganda na Rwanda kuhusu ujenzi wa reli na bomba la mafuta bila kufahamu kwamba ilikuwa inavunja misingi ya jumuiya hiyo.


Ni kufuatia hotuba aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusu hali tete iliyoanza kujitokeza katika Jumuiya hiyo inayojumuisha nchi Tano.
Dar es Salaam. Ikiwa ni siku nne baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge mjini Dodoma akilalamikia kutengwa na nchi washirika Afrika Mashariki,Kenya imekuwa ya kwanza kutamka hadharani kushirikiana na Tanzania.
Rais Kikwete katika hotuba yake,alielezea kushangazwa na washirika wenza wa Afrika Mashariki,Kenya,Uganda na Rwanda kufanya mikutano ‘kimyakimya’ bila kuwashirikisha.
Inadaiwa baada ya mkutano wa Aprili 28,mwaka huu mjini Arusha,wakuu hao wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda walikutana kimyakimya Juni 25 na 26,Entebbe nchini Uganda kabla ya kukutana tena Oktoba 28, Mjini Kigali,Rwanda katika mkutano waliouita “coalition of the willing”(Ushirikiano wa hiyari) wenye nia ya ujenzi wa Afrika Mashariki mpya.
Kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje wa Kenya, Amina Mohamed, Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu akisema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania na kwamba  walijiingiza katika mazungumzo yake na Uganda na Rwanda kuhusu ujenzi wa reli na bomba la mafuta bila kufahamu kwamba ilikuwa inavunja misingi ya jumuiya hiyo.
 Salamu hizo zilizowasilishwa na waziri huyo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,alisema kuwa hawaoni sababu hasa ya kuitenga Tanzania hasa kwa suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).
Waziri Amina aliyewasili nchini juzi kuzungumzia ushirikiano huo alisema, Tanzania na Kenya ndiyo waasisi wa EAC hivyo hawawezi kuacha ife.
Cuf watoa neno
Chama cha Wananchi (Cuf),kimesema Tanzania itazame na kuzirekebisha kasoro zinazosababisha nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuamua kuitenga badala ya kulalamika na kutafuta huruma.
Mwenyekiti wa Cuf, Profesa ,Lipumba alisema kumekuwa na kasoro mbalimbali zinazosababisha Tanzania kulalamikiwa na kufikiriwa kukimbiwa.
Alisema taarifa kuhusu uamuzi wa nchi za Rwanda na Uganda kutotumia Bandari ya Dar es Salaam lisitazamwe kisiasa badala yake iangalia udhaifu na upungufu uliopo katika bandari hiyo.
“Rwanda na Uganda si pekee wanaolalamikia Bandari ya Dar es Salaam bali wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi zikiwamo Kongo, Zambia na Malawi nao wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu.”
READ MORE THIS STORY: mwananchi
SOURCE: MWANANCHI