Wednesday 30 October 2013

Mkuu wa shule asakwa kwa udanganyifu


Na Brand Nelson, Mwananchi

Posted  Jumatano,Oktoba30  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alitoa agizo hilo jana alipotembelea shule hiyo kujua ukweli, ambapo pia aliagiza wanafunzi sita wa kidato cha tatu walioshirikiana na mwalimu huyo kusimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana ili kupisha uchunguzi


Mbeya.Serikali imewaagiza polisi mkoani Mbeya kumsaka mahali popote alipo aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nazarene iliyopo jijini hapa(jina tunalo) kwa madai ya kufanya udanganyifu wakati wa Mitihani ya Taifa ya Kidato cha pili akiwashirikisha wanafunzi sita wa kidato cha tatu Oktoba 7 mwaka huu.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alitoa agizo hilo jana alipotembelea shule hiyo kujua ukweli, ambapo pia aliagiza wanafunzi sita wa kidato cha tatu walioshirikiana na mwalimu huyo kusimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana ili kupisha uchunguzi.Ilielezwa kwamba wanafunzi hao walikamatwa wakifanya mitihani ya kidato cha pili kwa kutumia majina bandia ambayo walidai walipewa na mkuu wao wa shule na wala hayakuwa ya wanafunzi wa shule hiyo.

Baada ya wasimamizi wa mitihani kuwakamata wanafunzi hao, ilielezwa kwamba mkuu wa shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa la Nazarene la Kenya alitoweka na hadi sasa hajulikani aliko.

SOURCE: MWANANCHI