Thursday 31 October 2013

Hukumu ya Nguza Viking maarufu kama babu Seya imeanza kupitiwa.

 
 

 Mahakama ya rufaa imeanza kupitia hukumu ya mwanamuziki  maarufu  nchini mwenye asili ya jamhuri ya  kidemokrasia  ya congo  DRC Nguza Viking  maarufu kama Babu seya  na mwanawe Johnson  Nguza maarufu kama Papii kocha.

Mapitio  hayo yanafanywa na jopo la majaji  watatu wakiongozwa na Mh Nathali Kimaro amboa ndio waliotoa hukumu  Februari  2010 kwa upande wa waleta maombi wakiongozwa na wakili Mabetre Marando wamewasilisha mahakamani hapo mambo sita ambayo wangepedwa mahakama hiyo iyaangaliye kwa makini,ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi mashahidu muhimu hawakuitwa kutoa ushaidi wao.

Aidha wanataka ushaidi wa watoto uliotolewe katika kesi hiyo uondolewe katika kumbukumbu kwa sababu haukufuta taratibu na vigezo vya matwakwa ya sheria  ya ushaidi pia  wamesema kuwa katika ushaidi uliotolewa  ulionyesha kuwa  katika nyumba  ya babu seya  kulikuwa na  mlango wa siri lakini mahakama ilipokwenda hapo mlango huo haukuonekana.

Kwa upande  wa serikali kupitia wakili wake mwandamizi jackson burashi wameiomba mahakma hiyo kutupilia mbali  shauri hilo kutokana na ukweli kuwa yapo hapo kinyume na sheria  na yameletwa kama  rufaa  na siyo mapitio.

Aidha akaongeza kuwa maombi hayo hayajakidhi viwango vya sababu za mapitio kwa kuwa maombi hayo yalipaswa kuonyesha kuwa kosa limetendeka na haki ya mleta rufaa imepotea. Baada ya maelezo ya pande zote mbili mahakama ikasema itatoa maamuazi baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili

Babu Seya na mwanaye papii kocha wanaendelea kutumikia  kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na  hati  ya  makosa  ya kunajisi  na kulawiti  watoto wadogo kupitia huku iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu mwaka 2004  ambapo walihkumiwa kifungo cha maisha.

SOURCE: IPPMEDIA