Monday 28 October 2013

Balozi Sepetu afariki dunia D’Salaam



Na Mwandishi Wetu, Mwananchi


Posted  Jumatatu,Oktoba28  2013  saa 10:30 AM
Kwa ufupi
Hadi umauti unamkuta, Balozi Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar na Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki


Dar es Salaam. Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Isaack Sepetu, amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya TMJ Mikocheni, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Habari zilizopatikana jana zilisema marehemu Sepetu ambaye ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema, alilazwa hospitalini akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kupooza.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Zanzibar leo kwa ajili ya taratibu zote za mazishi
Hadi umauti unamkuta, Balozi Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar na Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.
Sepetu aliyetumia sehemu ya maisha yake Zanzibar, alimaliza masomo yake 1963 na kupata mafunzo mbalimbali nchini Ujerumani kabla ya kuteuliwa kuwa balozi  wa Tanzania katika nchi mbalimbali.

SOURCE: MWANANCHI