Saturday 28 September 2013

KINANA: Sina nywele kichwani kwa sababu ya kufikiria matatizo ya Watanzania!


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Ndg Abdulrahaman Kinana


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Ndg Abdulrahaman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma juzi amesema kuwa hapati usingizi kwa kufikiria matatizo ya watanzania hatua iliyosababisha hata nywele zake kuisha kichwani.

"Nina uchungu na matatizo yanayowakabili watanzania na nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi na hata kukosa usingizi kwa kufikiria namna ya kukabiliana na matatizo hayo,sina hata nywele kichwani kwa sababu hiyo"

Katika mkutano huo Kinana alihutubia kwa tahadhari kubwa akiepuka kutumia maneno ambayo yangewakwaza wananchi wa Musoma.

Tofauti na ilivyozoeleka alitumia zaidi neno wapinzani na kukwepa kuitaja Chadema.

SOURCE: MAISHA TIMES