Monday 30 September 2013

Jeshi la Polisi limesema litalinda Benki zote Jijini Dar Es Salaam kuanzia leo.


 


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeagiza makamanda wote wa mikoa mitatu kuanza kuweka askari polisi wenye silaha katika benki zote  ili kuimarisha ulinzi dhidi ya matukio wa wizi wa fedha yanajitokeza kwa kasi katika taasisi hizo za fedha jijini Dar es salaam.
Agizo hilo limetolewa na kamanda wa polisi Kanda maalum Suleiman Kova wakati alipozungumza na waaandishi wa habari,ambapo amesema  uchunguzi wa matukio ya wizi wa fedha katika mabenki umeonyesha kuwepo kwa njama za dhahiri kati ya wahalifu na watumishi na hata walinzi wa kampuni binafsi, na kusisitiza benki zote zitalazimika kufuata taratibu zilizowekwa na benki kuu ili kuhakikisha siri za benki hazivuji kwa wahalifu kama ilivyosasa.
Aidha kamishna Kova amesema Jeshi la Polisi limelazimika kuchukua hatua hizo kutokana na matukio hayo kuendelea kujirudia na kuhatarisha uwekezaji ambao pia unaingia katika mfumo mzima wa kukuza uchumi kwa Watanzania na kusisitiza jeshi hilo litahakikisha mtandao wa wizi huo wa Mabenki unakomeshwa ikiwa ni pamoja na kuwakamata wanaotoa taarifa za benki ili kusaidia hujuma zinazofanywa na kundi la wahalifu.

SOURCE: ITV -DAIMA