Tuesday 27 August 2013

*WAZIRI WA NISHATI NAMADINI PROF. MUHONGO AKAGUA MAENDELEO YA UTANDAZAJI MABOMBA YA GESI MTWARA-DAR

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
 Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
 Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
 Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
 Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
 Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na baadhi ya vibarua  wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji, Pwani.
 Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
 Mmiliki wa blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
 Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
 Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama, zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani Mkuranga, Pwani
Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa baharini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.