Saturday 31 August 2013

Putin ataka Marekani ioneshe ushahidi


 31 Agosti, 2013 - Saa 15:07 GMT

                               Putin
Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema tuhuma kuwa serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali ni upuuzi mtupu.
Anasema jeshi la Syria lilikuwa linasonga mbele, hapakuwa na sababu ya serikali kuwapa kisingizio wale wanaotaka kuingia kijeshi.
Bwana Putin alisema ikiwa Marekani ina ushahidi kuthibitisha tuhuma zake, basi ikabidhi ushahidi huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Alimkumbusha Rais Obama kuwa aliwahi kutunzwa tuzo ya amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio.
Alikaribisha uamuzi wa bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema ameshangazwa na uamuzi huo wa bunge.