Tuesday 27 August 2013

MHE. JERRY SLAA HAPA VIPI? MANDHARI SAFI, BARABARA SASA?



 Jitihada za Mhe. Meya wa Ilala, Jerry Slaa, zinaonekana jinsi anavyojitahidi kupendezesha Jiji na hasa katika Manispaa yake ya Ilala kwa kuweka Vivutio kadhaa katika baadhi ya makutano ya barabara au mizunguko ya Barabara, jambo ambalo ni zuri na utambulisho pekee kwa dereve yeyote kutambua kuwa sasa ameingia katika anga za Manispaa ya Ilala. 
Lakini katika eneo hili la mzunguko huu wa makutano ya Barabara ya Jamhuri, eneo hili limeharibika sana kutokana na kutawaliwa na mashimo ambayo kwa uhakika yanapoteza maana yote ya mapambo haya yaliyowekwa eneo hili. Au tutafsiri kuwa yameacha kwa makusudi ili kila atakayepita eneo hili aweze kupunguza mwendo kwa staili ya kuogopa mashimo kumbe ndo anashangaa mapambo haya??????
Magari yote yakifika eneo hili ni lazima yapunguze mwendo ili kukwepa mashimo haya, jambo ambalo linasababisha msongamano mkubwa wa magari katika eneo hili. Mhe. Jerry Slaa, tunajua unamajukumu mengi mbele yako ya kila siku lakini hebu jitolee kwa hili pia basi kwa kufukia mashimo haya ili uweze kufikisha ujumbe kamili kwa kila anayepita eneo hili. Yangu ni hayo tu.