Friday 30 August 2013

Halmashauri yakusanya Sh22 bilioni miezi 12


Na Gasper Andrew  (email the author)

Posted  Alhamisi,Agosti29  2013  saa 21:57 PM
Kwa ufupi
Mwenda alisema katika vyanzo vya ndani, halmashauri ilikusanya zaidi ya Sh419,000,000.


Singida. Halmashauri ya Wilaya ya Singida, imekusanya mapato ya zaidi ya Sh 22.9 bilioni kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ndani ya kipindi kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Illuminata Mwenda katika taarifa yake kuhusu mapato na matumizi.
Taarifa hiyo iliwasilishwa katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Singida.
Alisema makusanyo hayoni sawa na asilimia 78 ya lengo la kukusanya Sh29,583,444,380 katika mwaka huo wa fedha.
Mwenda alisema katika vyanzo vya ndani, halmashauri ilikusanya zaidi ya Sh419,000,000.
“Serikali kuu imetupatia zaidi ya Sh 515.4 milioni zikiwa ni ruzuku kwa vyanzo vya mapato vilivyofutwa,” alisema.
Katika hatua nyingine, kikao hicho kimeagiza mkaguzi wa mahesabu wa ndani, afanye ukaguzi wa vitabu vya kukusanyia mapato kwa watendaji wote wa kata.
Pia amkague kwa makini afisa mapato wa halmashauri hiyo, anayehusika na utoaji wa vitabu vya kukusanyia mapato.
source : Mwananchi