Thursday 25 July 2013

Sitta amtaka CAG achunguze ufisadi wa Sh8 bil ujio wa marais

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Baraza la Vijana (TYC) wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya, Dar es Salaam jana. 


Posted  Jumatano,Julai24  2013  saa 19:57 PM
Kwa ufupi
kuongeza: “Hivi sasa uchunguzi unaendelea, lakini hatuwezi kuwa kila siku ni uchunguzi tu na wakati mwingine uchunguzi umekuwa hauna matokeo.”


kuongeza: “Hivi sasa uchunguzi unaendelea, lakini hatuwezi kuwa kila siku ni uchunguzi tu na wakati mwingine uchunguzi umekuwa hauna matokeo.”
Alisema watumishi kama hao hawafai kwa kuwa wanatumia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha wao binafsi.
Mkutano wa Smart Partnership Dialogue ulifanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Julai Mosi mwaka huu.
Alisema walifahamu kuhusu ufisadi huo baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kueleza kuwa kuna utata kwenye fedha hizo na kwamba kampuni tatu hewa zililipwa fedha wakati hazijasajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).
“Kuna kampuni kama tatu, hizi nasikia zimeshachukuliwa hatua kwa kuwa ni hewa lakini bado... lazima CAG afanye ukaguzi kwa hizo Sh8 bilioni,” alisema Sitta.
Sitta ambaye amekuwa akijipambanua kuwa ni mmoja wa kundi la viongozi wanaopinga ufisadi, alisema watumishi wa jinsi hiyo, hawafai kwa kuwa wanatumia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha binafsi.
“Pamoja na yote, kampuni zina watu, lazima na wao wachukuliwe hatua. Wahusika wote ninaamini wanafahamika sasa isifikie hatua tunaambiwa uchunguzi usiofikia mwisho,” alisema Sitta.
Hata hivyo, Balozi Sefue hakupatikana jana kuelezea tuhuma hizo ambazo hivi karibuni ziliripotiwa na gazeti moja la kila wiki kwani simu yake iliita bila ya majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu na baadaye simu yake haikuwa tena hewani.
Aendelea kuponda Serikali Tatu
Sitta aliendelea na msimamo wake wa kupinga mapendekezo ya Tanzania kuwa na Serikali Tatu akisema wanaopigania hilo wana masilahi binafsi.
Sitta ambaye aliwahi pia kuwa Spika wa Bunge, alishawahi kutoa msimamo wake kuhusu Serikali Tatu kama zilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Rasimu ya Katiba akisema hakuna nchi duniani yenye utawala wa marais watatu na endapo Tanzania itakuwa hivyo, itaweka rekodi ya kuwa ya kwanza.
Sitta ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaotaka kuwania urais mwaka 2015, alisema Katiba ina masilahi ya watu aina mbalimbali lakini hatari anayoiona ni kwa wale wenye masilahi binafsi ambao wanaweza kuathiri mchakato huo kwa kuwa wanafikiria urais.

“Tunaweza kuwa na Serikali Tatu bila kuwa na marais watatu. Tukiwa na Serikali Tatu tuwe na rais mmoja na labda naibu rais au makamu wa rais au waziri mkuu, haiwezekani tukawa na marais watatu kwani hiyo ni gharama kubwa,” alisema. “Kuna wakati nilisema hiki ni kioja fikiria rais anasafiri kwenda nje halafu unasikia huyu ni wa Tanganyika huyu ni wa Muungano na huyu ni wa Zanzibar hata watu watatushangaa.”
Aidha, Sitta aliwaambia vijana hao kuwa hakubaliani na pendekezo la kuwa na mawaziri 15 katika Serikali ya Muungano.
“Utakuwaje na mawaziri 15 na wabunge wengi kujadili mambo saba ya Muungano? Kwa nini tusiwe na mawaziri saba kwa ajili ya kusimamia mambo hayo?”
Alisema ni vyema vijana wakajadili hayo mambo kwa kuwa ni wao watakaonufaika au kinyume chake na Katiba Mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba walio na umri wa chini ya miaka 35 nchini ni asilimia 70.
Waziri Sitta alisema vijana wanahitaji kuwezeshwa zaidi kwa kuwa mchakato wa Katiba Mpya bado ni mrefu na wao ndio wanatakiwa kufaidika nao.
Alisema baadhi ya viongozi wa kijamii na kisiasa ambao ni walafi wamekuwa wakiwanunua kwa masilahi yao binafsi... “Vijana wa Tanzania ni baridi sana kwani baadhi yenu mnakubali kununuliwa kitu ambacho ni hatari kwa kuwa mnakaribisha Tanzania isiyotawalika.” “Haiwezekani nchi ina wenye uwezo kupita kiasi huku wengine wakiwa hohehahe, lazima vijana muwe wanaharakati wa kupigania utawala bora na kuiepusha nchi isije ikaingia kwenye matatizo ya kutokuwa na amani.”

chanzo: Mwnanachi news paper