Wednesday 24 July 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Na  Mwandishi wetu.
Julai 23,2013.
Jana, Rais J. Kkikwete alikutana na viongozi wa chama cha makampuni ya simu na kuzungumza kwa kina juu ya pendekezo la simu kadi. Pendekezo hili limezua gumzo na sintofahamu miongoni mwa wananchi wengi na wengi wao wakiwa wa kipatao cha chini.
Inaonekana serikali inaelekea kushindwa kutetea hoja yake ya kuanzisha kodi hiyo. Ina imeripotiwa kuwa Raisi ametoa wito wa wadau wote kuliangalia upya swala hili kwa upana na kwa haraka.


vo1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013

vo2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 2
vo3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na  wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazuangumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
PICHA NA IKULU