Monday 22 July 2013

PICHA: MIILI YA ASKARI 7 WA JWTZ WALIOUAWA DARFUR ILIPOWASILI DAR

Wanajeshi wa JWTZ wakibeba jeneza lenye mmoja wa askari wenzao saba waliouawa kwa shambulio la ghafla wakiwa katika Jeshi la Ulinzi wa Amani la Umoja wa Mataifa mjini Darfur, jumamosi iliyopita. Miili hiyo iliwasili leo Jumamosi, tarehe 20, saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga cha JWTZ.
Baadhi ya viongozi wakiongozwa na Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal wakishuhudia miili ya wanajeshi saba wa JWTZ waliouawa na waasi mjini Darfur, miili hiyo ilipofikishwa leo Uwanja wa Ndeje wa Kikosi cha anga cha JWTZ jijini Dar es Salaam.
Askari wakiingiza mwili mmoja wapo kati ya miili saba katika gari la jeshi tayari kuisafirisha.
Baadhi ya wananchi wakiwa hawaamini wanchokiona

 Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Job Masima wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga cha JWTZ, kabla ya miili kuwasili. Wengine kulia ni Ridhiwani Jakaya Kikwete, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba. ambao walihudhuria mapokezi ya miili hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Mstaafu, Abdurhaman Kinana, baada ya kuwasili kwenye mapokezi ya miili ya wanajeshi hao. Katikati ni Waziri wa Ulinzi Shamshi Vuai Nahodha
 Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauyebaada ya kuwasili kwenye Mapokezi ya miili ya askari wa JWTZ waliouawa mjini Darfur

Makamu wa Rais, Dk. Muhamed Gharib Bilal akiagana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, baada ya mapokezi ya wanajeshi wa JWTZ waliouawa Darfur kukamilika
 
 Ndugu wa mmoja wa askari wa JWTZ waliopoteza maisha kwa kushambuliwa na waasi mjini Darfur akiwa mwenye majozi wakati wa mapokezi ya askari hao.
Msafara wa malori saba yaliyobeba miili ya askari saba wa JWTZ waliouwa Darfur uliongozwa na polisi wakati wa kutoka Uwanja wa Ndege, Kikosi cha Anga baada ya kupokewa leo jioni. 
Picha zote na theNkoromo Blog