Thursday 18 July 2013

Kisumo: Mbowe acha kuitumbukiza nchi yetu kwenye uvunjifu wa amani

                  

“Unaposema huna imani na JWTZ, Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda tafsiri yake ni kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” Peter Kisumo 
Na Daniel Mjema, Mwananchi  (email the author)

Posted  Jumatano,Julai17  2013  saa 10:25 AM
Kwa ufupi
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko hizo.


Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo, amemvaa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akimtaka aache kile alichodai ni kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.
 “Unaposema huna imani na JWTZ, huna imani na Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda tafsiri yake ni kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” alisema.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko hizo.
“Zipo nchi zina mapesa mengi na zipo tayari kufadhili machafuko nchi nyingine lakini nchi zilizostaarabika kama Ujerumani, Marekani, Uingereza na nyingine haziwezi kujiingiza huko,” alisema.
Alisema anaamini hata Ujerumani ambayo imekuwa ikikifadhili Chadema, haitakubali kutoa fedha kufadhili uanzishwaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wakati vyombo halali vya ulinzi ni Polisi na JWTZ.
Kisumo alifafanua kuwa vyama vya siasa vina sare zake na kusema CCM, Chadema na Cuf navyo vina sare lakini kutaka kuanzisha vikundi vya ulinzi inamaanisha vitapaswa kuwa na sare za kijeshi.
  Kwa mujibu wa Kisumo, anaamini vyombo vya ulinzi na usalama nchini havitaruhusu kutekelezwa kwa mpango huo kwani unalenga kuwachochea wafuasi wa Chadema kutokutii mamlaka ya dola.
Suala la Chadema kutangaza mpango wake wa kuanzisha vikundi vya ulinzi limeibua mjadala mkali kati yake na CCM ambacho kinamiliki kikundi cha Green Guard huku Chadema wakimiliki Red Brigad