Wednesday 5 June 2013

SHEREHE YA KUWAAGA WENZETU IMEWADIA-08.06.2013

Napenda kuwakumbusha Ndugu na jamaa wote wa hapa mjini Oslo na maeneo mengine kuwa party ya kuwaaga ndugu zetu wanaohitimu kutoka vyuo mbalimbali hapa Nchini Norway imewadia, itakuwa tarehe 08.06.2013.

Tunakumbushwa kufika mapema ili tuwe na muda wa kuburudika zaidi kwa pamoja.
Kwa wale ambao bado hawajatoa michango ya uanachama wajitahidi watoe ili tuwe na sherehe nzuri na ya kupendeza.
Pamoja na hayo pia, tutawakuwa na Dr. L. Lwaitama ambae atakuwa na machache ya kutueleza. Kwa wale waliopitia chuo kikuu cha Dar es Salaam bila shaka huyu Mwalimu anajulikana vizuri.

Natanguliza shukrani kwenu kwa ushirikiano wenu.

PRO