Friday 21 June 2013

IDD SIMBA afutiwa kesi ya UDA


 
Na Tausi Ally  (email the author)

Posted  Jumatano,Juni19  2013  saa 20:45 PM
Kwa ufupi
  • DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja kujenga kesi yake anatumia kifungu hicho kufuta kesi kwani kuendelea kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahidi thabiti wa kuwaleta mahakamani ni matumizi mabaya ya sheria na kuisababishia Serikali gharama pamoja na mrundikano wa kesi mahakamani


kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini Wakili wa Serikali, Awamu Mbangwa aliwasilisha hati hiyo, chini ya Kifungu cha 91 (1) cha Mashauri ya Jinai (CPA), kwa niaba ya DPP akiomba kesi hiyo ifutwe kwa sababu hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao.
Baada ya kuwasilisha hati hiyo, Hakimu Mugeta alikubaliana na ombi hilo na kuifuta. Mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Alex Mgongolwa alisema hawana pingamizi la kufutwa kwa shauri hilo ingawa walitaka waelezwe sababu za hatua hiyo.
Mgongolwa alisema walitaka kujua sababu hizo kwani walikuwa na wasiwasi kuwa wateja wao wangeachiwa huru na kukamatwa tena baada ya muda mfupi na kupandishwa kizimbani.
Kutokana na shaka hiyo, waliiomba Mahakama kuwapa kinga.
Akiifuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 3/2013 na kuwaachia huru washtakiwa hao ambao ni Simba na wenzake, Salum Mwaking’inda na Meneja wa Shirika hilo, Victor Milanzi, Hakimu Mugeta alisema maombi ya upande wa mashtaka yamekubaliwa.
Akizungumzia uamuzi huo wa DPP wa kuwafutia kesi wateja wake, nje ya viwanja vya mahakama hiyo, Wakili Mgongolwa alipongeza uamuzi huo akisema ni matumizi ya sheria.
“DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja kujenga kesi yake anatumia kifungu hicho kufuta kesi kwani kuendelea kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahidi thabiti wa kuwaleta mahakamani ni matumizi mabaya ya sheria na kuisababishia Serikali gharama pamoja na mrundikano wa kesi mahakamani,” alisema Mgongolwa.
Mapema Aprili 30, mwaka huu, upande wa mashtaka uliifuta kesi ya awali ya matumizi mabaya ya madaraka iliyokuwa ikimkabili Simba na wenzake wawili na kisha kuwafungulia kesi nyingine ya mashtaka sita ya rushwa na uhujumu uchumi. Katika kesi hiyo namba 3 ya 2013, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kughushi. Walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Mei 29, 2012 kujibu shtaka la kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh8.4 bilioni.
Walidaiwa kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, walikula njama za kutenda kosa la vitendo vya rushwa, kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Pia walidaiwa kufanya vitendo vya rushwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010 kwa kukubali kupokea Sh320 milioni kama ushawishi wa kuiuzia Simon Group hisa za Uda ambazo zilikuwa hazijagawiwa.