Tuesday 18 June 2013

DAU MIL 100 KWA MTU ATAKAYE WEZESHA KUPATIKANA KWA MLIPUAJI WA BOMU


 Arusha.
Serikali imetangaza kutoa zawadi ya Shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa washukiwa wa milipuko ya mabomu inaoendelea mara kwa mara katika siku za hivi karibuni sasa nchini.

Jeshi la polisi nchini limeepiga marufuku mikusanyiko ya watu mkoani Arusha wakati huu jeshi hilo likiendelea kufanya uchunguzi wa mlipuko wa bomu uliotokea mishoni mwa wiki huko Soweto,
Arusha.

Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais, Dkt. M. G. Bilal, na Waziri Mkuu M. P. Pinda, hii leo walizuru eneo palimotokea mlipuko na kutoa ahadi ya kutafuta kiini cha tukio hilo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa Freeman Mbowe amesema watatoa ushirikiano endapo uchunguzi wa mlipuko huo utafanywa na vyombo vingine nje ya jeshi la polisi ambalo wamekosa imani nalo.

Wakati jeshi la polisi na vyombo mbalimbali vya usalama vikihaha kumtafuta m/wahusika wa bomu hilo, Katibu wa Uenezi Taifa wa CCM, Nape Nnauye amesema CCM inakituhumu moja kwa moja Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo wahusika.

Baadhi ya Wabunge wametoa maoni yao Bungeni leo wakitaka uchunguzi ufanywe na ikibainika kuwa vyama vya CHADEMA na CCM vinahusika na matukio haya, wanamshauri msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania alazimike kuvifuta kwa kile walichosema kuwa, “Tanzania ni zaidi ya vyama hivi viwili.”

Hadi sasa watu watatu wanaripotiwa kufa kutokana na mlipuko huo, huku wengine 68 wakiachwa na majeraha, baadhi yao wakiwa mahospitalini bado na miongoni mwao kupelekwa nje ya nchi, Nairobi, Kenya, kwa matibabu zaidi.

Hayo na mengine mengi yapo katika audio na video za taarifa mbalimbali zilizopachikwa hapo chini.