Saturday 22 September 2012



KUHUSU KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WAPYA KATIKA CHAMA CHA TASAO(TANZANIA STUDENT ASSOCIATION IN OSLO)

Tarehe 22/08/2012 jumuyia ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Oslo, Norway wamekuta na kuwakaribisha wanafunzi wapya waliokuja kusoma shahada mbalimbali.

Mhe Rais wa TASAO Mchg. Godrick Lyimo alichakuwa nafasi ya kuwakaribisha wanafunzi hao waliokuja masomoni mwaka huu wa wa masaomo 2012/13. Mhe. Rais aliwapongeza sana wanafunzi hao kwa kupata nafasi ya kuja kusoma Norway, nafasi ambayo sio kila mtu anapata, Mhe Rais pia aliwaambia wanafunzi wapya malengo na madhumuni ya kuwepo kwa chama cha TASAO kuwa ni kujenga umoja wa wanafunzi wa Kitanzania ili waweze kusaidiana wakati wa shida na wa raha, kukaa kama ndugu wakiwa nje ya nchi yao. Mhe Rais aliwaomba wanafunzi wote wapya na wa zamani waendelee kushikamana na kusaidiana kama ndugu maana Tanzania ni moja na watu wake ni wamoja.


Pia Rais mstaafu Mhe Doreen Ndosi alipata naye wasaa wa kuwashauri wanafunzi wote wa TASAO juu ya maisha ya Oslo, jinsi watakavyoishi na kutimiza lengo walilolijia ambalo ni kusoma, aliwataka wanafunzi wote wapya na wanaondelea waliweke jina la Tanzania ktk nafasi nzuri wakiwa nje ya nchi. Aliongeza pia kuwa wana TASAO wasaidiane kama ndugu wakati wa shida na raha pia.

Mwisho, tafrija hiyo fupi ya kukaribishana ilifungwa kwa neno la shukrani na Mchg. Samson Olodi Laiser, naye aliwashukuru wote kwa mahudhurio mazuri, na pia aliwashukuru kamati ndogo iliyaandaa tafrija hiyo na wale waliotoa ukumbi wa sherehe.