Friday, 31 December 2010

TAARIFA YA MSIBA

Habari watanzania wenzangu!

Nachukua nafasi hii kuwapa taarifa kuwa ndugu yetu Marcelin Raphael Ndimbwa amefiwa na baba yake mzazi huko Mbeya leo asubuhi saa 12. Taarifa zaidi za mazishi tutaendelea kufahamishana.

Hivyo tujumuike pamoja katika kumfariji mwenzetu kwa hali na mali na kumuombea ili aweze kumpumzisha salama baba yetu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Amina!

Fatuma Hussein.