Friday, 16 February 2007

ZIARA YA J.K. OSLO (ni kama email hapo chini inavyosomeka)


Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Date: Fri, 16 Feb 2007 21:13:51 +0000 (GMT)
From: "Semboja, Mohamed Jumanne"
Subject: Kukutana na Kikwete, Grand Hotel Oslo Norway.
To: "Tanzanet" , "Tanzanet"
CC: "Embassy of Tanzania Stockholm" , norwaytanzanian@googlegroups.com
Taarifa toka ubalozi wetu Stockholm (Sweden) http://www.tanemb.se/

Rais Jakaya Kikwete atakutana na Watanzania waishio Norway hapa Oslo.

Jumatano: Tarehe 28. Februari 2007

MAHALI: Grand Hotel, Karl Johan avenue, Oslo. Karibu na Bunge la Norway (Stortinget)

Saa: Mlango utakuwa wazi saa 17.00 - 18.30 Central European Time.

Baada ya hapo mlango utafungwa! Tukimsubiri Rais.

Tafadhali toa taarifa hii kwa Mtanzania/Watanzania unayem/wafahamu aishie/waishio Norway.

Mnaombwa kuzingatia muda, kufika kwa wakati na kukaa kabla ya Mheshimiwa Rais kuingia. Kuhusu mavazi, itapendeza tukiwa rasmi kwa vazi la heshima.

Ili kujua idadi ya watakaohudhuria tunaomba mpige simu Ubalozini namba +46 8 7322441 au +47 8 7322430 (Stockholm, Sweden) kujiandikisha. au piga simu namba hizo hapo chini, Oslo, Norway.

Wenu,


Semboja, Mwamedi Jumanne.
(Katibu),
Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo).

Baruapepe: tanzania@online.no
Baruapepe: tanzaniamail@yahoo.com
Simu ya chama ya mkononi: +47 90 80 69 01
Simu ya Semboja (mkononi): +47 95 78 21 96
Simu ya Semboja (nyumbani): +47 22 25 67 77

Saturday, 3 February 2007

MWANZO MZURI

Hawa ni mwenyekiti na katibu wa TASAO, bwana John na bi Alice. waheshimiwa hawa wanastahili pongezi kwa kazi kubwa wanayofanya kwa TASAO. watakuwepo madarakani mpaka hapo mkutano mkuu utakapo wachagua m/kiti na katibu kwa mujibu wa katiba iliyopitishwa na mkutano mkuu wa leo. hii ni dondoo tu, habari kamili itatolewa na katibu. anayewaletea dondoo hizi ni Joshua.

WANA-TASAO WAKIMSIKILIZA KATIBU

Hii ni sehemu ya wana-tasao wachache waliohudhuria kikao cha leo, hapa wanaonekana wakimsikiliza katibu (hayupo pichani) akiwabrief yaliyojiri kwenye kikao kilichopita. kikao kingine ni tar 24 mwezi wa pili, habari zaidi zitatolewa baadaye.

POLENI na Hongera sana vijana

Hawa hapo juu ndiyo waliofika kwenye eneo la kikao kama ilivyopangwa yaani saa saba na nusu.... walikuwa na kibarua cha kusubiri wengine kwa muda wa takribani saa moja. Nawapa pongezi na nawaomba wasomi wengine ku-keep muda. kutoka kushoto ni bwana John, Joshua na James (triple js).