Friday 16 February 2007

ZIARA YA J.K. OSLO (ni kama email hapo chini inavyosomeka)


Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Date: Fri, 16 Feb 2007 21:13:51 +0000 (GMT)
From: "Semboja, Mohamed Jumanne"
Subject: Kukutana na Kikwete, Grand Hotel Oslo Norway.
To: "Tanzanet" , "Tanzanet"
CC: "Embassy of Tanzania Stockholm" , norwaytanzanian@googlegroups.com
Taarifa toka ubalozi wetu Stockholm (Sweden) http://www.tanemb.se/

Rais Jakaya Kikwete atakutana na Watanzania waishio Norway hapa Oslo.

Jumatano: Tarehe 28. Februari 2007

MAHALI: Grand Hotel, Karl Johan avenue, Oslo. Karibu na Bunge la Norway (Stortinget)

Saa: Mlango utakuwa wazi saa 17.00 - 18.30 Central European Time.

Baada ya hapo mlango utafungwa! Tukimsubiri Rais.

Tafadhali toa taarifa hii kwa Mtanzania/Watanzania unayem/wafahamu aishie/waishio Norway.

Mnaombwa kuzingatia muda, kufika kwa wakati na kukaa kabla ya Mheshimiwa Rais kuingia. Kuhusu mavazi, itapendeza tukiwa rasmi kwa vazi la heshima.

Ili kujua idadi ya watakaohudhuria tunaomba mpige simu Ubalozini namba +46 8 7322441 au +47 8 7322430 (Stockholm, Sweden) kujiandikisha. au piga simu namba hizo hapo chini, Oslo, Norway.

Wenu,


Semboja, Mwamedi Jumanne.
(Katibu),
Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo).

Baruapepe: tanzania@online.no
Baruapepe: tanzaniamail@yahoo.com
Simu ya chama ya mkononi: +47 90 80 69 01
Simu ya Semboja (mkononi): +47 95 78 21 96
Simu ya Semboja (nyumbani): +47 22 25 67 77